Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Libya hali si shwari, baraza la Usalama laimarisha vikwazo vya silaha

Tarik Mitri, Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa UM nchini Libya, UNSMIL. (Picha:UN /Loey Felipe)

Libya hali si shwari, baraza la Usalama laimarisha vikwazo vya silaha

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha kwa kauli moja azimio la kupanua wigo wa vikwazo vya silaha nchiniLibyaikiwemo udhibiti zaidi kwenye taratibu za misamaha ya uingizaji silaha unaotumika hivi sasa.

Baada ya kupitishwa kwa azimio hilo Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Libya Tarik Mitri alihutubia baraza akisema kuwa mapigano yameendelea kwa mfululizo kwenye miji ya Tripoli na Beghazi na kwingineko huku yakichochewa na mashambulizi ya anga.

(Sauti ya Tarik)

Kitendo cha pande zote kutumia silaha nzito kushambulia maeneo ya wakazi wengi, kimeongeza hofu na vitendo vya ugaidi na kusababisha watu wengi wasio na hatia kupoteza maisha ikiwemo watoto. Halikadhalika kumekuwepo na matukio mengi ya utekaji nyara, uchomaji moto nyumba, uporaji na matukio mengine ya kulipiza visasi.”

Tarik ambaye anahitimisha jukumu lake la kuongoza ujumbe wa Umoja wa Mataifa hukoLibya, UNSMIL, amesema wao wanaamini kuwa ujumbe muafaka unapaswa kutumwa kwa pande zinazokinzana hukoLibyajuu ya wajibu wao  wa kuzingatia sheria za kimataifa za kibinadamu.

Amesisitiza umuhimu wa ushiriki wa dhati wa pande zinazokinzana kwenye mchakato wa kisiasa unaoratibiwa na Umoja wa Mataifa.