Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zaidi ya mashirika 900 yasiyo ya kiserikali yajadili ajenda ya maendeleo na UM

UN Photo/Violaine Martin
Maher Nasser, Kaimu Mkuu wa Idara ya Mawasiliano ya Umoja wa Mataifa. Picha:

Zaidi ya mashirika 900 yasiyo ya kiserikali yajadili ajenda ya maendeleo na UM

Wawakilishi wa Umoja wa Mataifa kupitia Idara yake ya mawasiliano, DPI kwa kushirikiana na zaidi ya mashirika 900 yasiyo ya kiserikali wanakutana kuanzia leo mjini New York kwa ajili ya kongamano maalum kuhusu ajenda ya maendeleo.

Maudhui ya mwaka huu ni ushirikiano wa jamii katika kuunda ajenda ya maendeleo endelevu ya baada  ya mwaka 2015.

Kwa mujibu wa Maher Nasser, Kaimu Mkuu wa Idara ya Mawasiliano ya Umoja wa Mataifa, mkutano huo ni wa msingi sana kwani utasaida kuhakikisha sauti ya kila mtu inasikika, hasa watu walio pembezoni.

(sauti ya Nasser)

“Kwa  Kawaida majadiliano ya  asasi za kiraia hayadhibitiwi kama ilivyo kwa nchi wanachama, na adhma zao  ni  kubwa zaidi na hiyo itakuwa na  matokeo makubwa. Na hayo hayapaswi kuishia hapo kwa kuwa ni majadiliano na malengo endelevu juu ya namana gani tunaunganisha asasi hizi  kimatifa kutusaidia kufikia malengo haya”

Mkutano huo unatakiwa kuchangia katika maandalizi ya mkutano mkuu wa Septemba 2015 ambapo malengo mapya ya maendeleo yataamuliwa.