Kongamano kuhusu Ebola laanza huko Congo-Brazavillle

27 Agosti 2014

Shirika la Afya Duniani, WHO limeendelea na harakati zake za kupambana na ugonjwa wa Ebola ambapo harakati za hivi karibuni zaidi ni warsha kuhusu ugonjwa huo lililoanza leo huko Congo-Brazaville ikijumuisha wataalamu zaidi ya 40. Taarifa zaidi na Abdullahi Boru.

(Taarifa ya Abdullahi)

Washiriki kutoka wizara za afya na wawakilishi wa WHO wanatoka  Botswana, Ethiopia, Ghana, Kenya, Namibia, Rwanda,Tanzania,Uganda,Zambia na Zimbabwe wanashiriki warsha hiyo iliyoanza hapo jana.

Mkurugenzi wa kitengo cha chanjo, kinga  kutoka WHO  Kanda ya Afrika, Dkt. Deo Nshimirimana amesema japo juhudi za kukabiliana Ebola zinafanyika, mlipuko wa ugonjwa huo unaendelea, na watu wengi wanazidi wanakufa au kuambukizwa, na kwa hivyo kuhatarisha maisha ya watu Afrika na uliwengu nzima.

Amesema  Ebola kwa sasa sio tatizo tu la kiafya , bali pia ni tisho kwa uchumi na maendeleo  ya mataifa yetu na kwa hivyo tunahitaji kuharakisha juhudi za kupambana nayo.

Katika hatua nyingine Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuweka utulivu huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC, MONUSCO,  imesema kuwa Umoja wa Mataifa umetoa msaada ya dola Millioni moja na nusu za kuisaidia  DRC kupambana na Ebola.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud