Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Waasi wa zamani wa JEM-SUDAN wanza kujumuishwa jeshini

Harakati za ujumwishaji wa JEM-SUDAN kwenye jeshi la kitaifa nchini Sudan El Fasher Kaskazini mwa Darfur.Picha@Photo by Hamid Abdulsalam, UNAMID.

Waasi wa zamani wa JEM-SUDAN wanza kujumuishwa jeshini

Takribani waasi 1,300 wa zamani wa kikundi cha JEM-SUDAN wamenza kujumuishwa kwenye jeshi la kitaifa nchini Sudan kufuatia hatua ya kikundi hicho kutia saini makubaliano ya Doha kuhusu amani Darfur, DDPD.

Ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika huko Darfur, UNAMID umesema hilo ni kundi la kwanza kutoka takribani askari 2700 ambao hatimaye watajiunga na jeshi la kawaida.

UNAMID imeelezea kuwa kitendo hicho kilichoshuhudiwa huko El Fasher ni hatua muhimu kwani kujumuishwa kweye jeshi la serikali ni kipengele muhimu katika makubaliano ya DOHA.

Luteni Jenerali Paul Mela ni Mkuu wa vikosi vya UNAMID na amezungumzia hatua hiyo.

(Sauti ya Lt. Jenerali Mela)