Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban asema sitisho la mapigano Gaza ni fursa ya amani ya kudumu

Shule ya Jabalia iliyopigwa na makombora awali. (Picha:Maktaba:UNRWA/Shareef Sarhan)

Ban asema sitisho la mapigano Gaza ni fursa ya amani ya kudumu

Ripoti  ya kwamba Israeli na Palestina zimefikia makubaliano yasiyo na ukomo kuhusu kusitisha mapigano zimeungwa mkono na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ambapo taarifa ya msemaji wake imemkariri akisema kuwa nuru ya ustawi kwaGazana Israeli yategemea sitisho endelevu la mapigano.

Ban amesema kilichobakia sasa baada ya jitihada za Misri ni kwa pande zote kuwajibika kwa kuzingatia makubaliano hayo.

Amesema baada ya mfululizo wa mauaji  na matukio mengi ya uharibifu wa makazi ya wapalestina, raia katika katika pande zote zinazohusika na mzozo huo wa Ukanda wa Gaza wanapaswa kusamehe ili kurejea katika maisha yao ya kawaida na huduma za kibiandamu ziweze kushika kasi.

Mathalani amesema watoto hukoGazana Israeli wanapaswa kuanza shule bila milio ya maroketi au mashambulio ya angani.

Katibu Mkuu Ban amesema bado ana matumain kuwa makubaliano hayo ya sasa yatakuwa ni kiashiria cha mchakato wa kisiasa ambao ndio njia pekee ya kufikia amani ya kudumu.

Ametaka pande zote kufanya mashauriano ya dhati ili kufikia makubaliano ya mwisho yatakayoshughulikia kina cha mzozo huo na kumaliza miaka 47 ya kukaliwa kwa eneo la Gaza.