Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lasikitishwa na maendeleo finyu dhidi ya FDLR

UN Photo/Loey Felipe/NICA
Kikao cha Baraza la Usalama.

Baraza la Usalama lasikitishwa na maendeleo finyu dhidi ya FDLR

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetoa taarifa ambayo pamoja na mambo mengine inakaribisha maendeleo yaliyopatikana dhidhi ya makundi yaliyojihami huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, ikiwemo kufurushwa kwa kundi la M23.

Hata hivyo Baraza hilo limesikitishwa na ukosefu wa maendeleo muhimu katika kutokomeza kundi la FDLR.

Kwa mantiki hiyo limeunga mkono hatua za kuvunja nguvu FDLR kama hatua muhimu ya kuleta utulivu nchini DRC na eneo zima la Maziwa Makuu.

Baraza hilo pia katika taarifa hiyo limetambua kuwa baadhi ya viongozi na wanachama wa FDLR walishiriki mauaji ya halaiki ya mwaka 1994 nchini Rwanda na kurejelea kuwa kundi hilo liko chini ya vikwazo vya Umoja wa Mataifa.