Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mafuriko yahatarisha afya ya wakimbizi wa ndani Bentiu

Watoto wakitembea ndani ya maji ya matope kufuatia mafuriko yaliyotokana na mvua kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani ya Bentiu, jimbo la Unity nchini Sudan Kusini. (Picha: UNMISS / JC Mcilwaine

Mafuriko yahatarisha afya ya wakimbizi wa ndani Bentiu

Nchini Sudan Kusini wakati harakati za kuleta amani zinaendelea, mapigano nayo kwenye maeneo ya makazi yanashika kasi na hivyo raia kusaka hifadhi kwenye kituo cha hifadhi kilichoandaliwa kwenye ofisi za ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS kwenye mji wa Bentiu, jimbo la Unity. Hata hivyo uwepo wa wakimbizi hao wa ndani kwenye eneo hilo unaingia mushkeli kutokana na mvua kubwa zilizosababisha mafuriko na hata kuweka hatari ya kupata magonjwa ya kuambukiza. Kaimu Mkuu wa UNMISS Toby Lanzer alifanya ziara eneo hilo kujionea hali halisi. Je kipi alishuhudia? Ungana na Assumpta Massoi kwenye makala hii.