Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ajali ya helikopta ya UNMISS yaua watatu huko Bentiu

Picha@UNMISS

Ajali ya helikopta ya UNMISS yaua watatu huko Bentiu

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa huko Sudan Kusini UNMISS umethibitisha kuwa watu watatu waliokuwa wameajiriwa na Umoja huo na wakifanya kazi katika  helikopta yake aina ya MI-8 wamefariki dunia leo mchana na mwingine amejeruhiwa baada ya helikopta hiyo kuanguka karibu na mji wa Bentiu, jimbo la Unity.

Taarifa ya UNMISS inasema majeruhi huyo sasa anapatiwa tiba na jopo la wahudumu wa afya huko Bentiu.

Kaimu Mkuu wa UNMISS Toby Lanzer ametuma salamu za rambirambi kwa familia za wafiwa na akimtakia ahueni ya haraka majeruhi wa ajali hiyo huku akisema kuwa wameanza uchunguzi wa kina dhidi ya tukiohilo.

Helikopta hiyo ikiwa na shehena ilikuwa katika safari zake za kawaida ikitoka Wau jimbo la Magharibi laBahr El Ghazalkuelekea Bentiu na UNMISS inasema ilipoteza mawasiliano majira ya saa Nane Na nusu adhuhuri kwa saa za Sudan Kusini.