UNICEF yatoa msaada mkubwa zaidi kuwa kutoa ndani ya mwezi mmoja

26 Agosti 2014

Mwezi huu wa Agosti, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limetuma misaada ya zaidi ya tani Elfu Moja kwa ajili ya kuokoa maisha ya watoto waliokubwa na dharura kwenye maeneo ya mizozo. Taarifa zaidi na Abdullahi Boru.

(Taarifa ya Abdullahi)

Msaada huo ni kiwango kikubwa zaidi kuwahi kutolewa na UNICEF katika kipindi cha mwezi mmoja kwenye historia ya shirika hilo.

Mkurugenzi Mkuu wa operesheni za usambazaji na usafirishaji misaada Shanelle Hall amesema usafarishaji mkubwa huu wa UNICEF umetokana na mahitaji kutoka mataifa mengi kwa wakati mmoja.

Misaada hiyo imepelekwa Jamhuri ya AfriKa ya Kati, Iraq, Liberia, Palestina, Sudan Kusini na Syria.

Kwa kutambua mapema mahitaji kufuatia mapigano nchiniIraqna kuzuka kwa ugonjwa wa Ebola Afrika Magharibi, UNICEF ilikodisha ndege nyingi za kuwezesha kusafirisha shehena hizo.

Halikadhalika UNICEF imepeleka misaada ya huduma za afya, lishe bora pamoja na  huduma ya afya ya uzazi kwa wakimbizi wa Syriawalioko katika kambi ya wakimbizi walioko Azraq and Zaatari.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter