Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban anafautilia hali ya Sudan Kusini

Kambi ya wakimbizi wa ndani katika kituo cha UNMISS.Picha/UNMISS/JC McIlwaine/NICA

Ban anafautilia hali ya Sudan Kusini

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekaribisha mkutano wa Jumatatu wa viongozi wa nchi watendaji wa IGAD kuhusu Sudan Kusini.

Taarifa ya msemaji wa katibu Mkuu imemkariri Ban akisema kuwa anatambua kutiwa saini kwa makubaliano ya kumaliza uhasama yaliyofikiwa Januari mwaka huu kati ya serikali ya Sudan Kusini na vikosi vilivyoasi kutoka jeshi la serikali SPLA.

Amezitaka pande zote kutekeleza makubaliano ya usitishaji mapigano kama ilivyokubaliwa na pande zote kwenye mzozo wa Sudan Kusini na kuonyesha mshikamano wao katika kuunda serikali ya mpito yenye umoja.

Katibu Mkuu huyo amewapongeza watendaji wa IGAD na wawakilishi wao katika juhudi zao za kutafuta suluhu kwa mzozo wa Sudan Kusini na kuhimiza mshikamano wa Umoja wa Mataifa katika juhudi hizo.