Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kamati ya UN juu ya haki za watoto kuzitathmini nchi wanachama

Watoto katika moja ya kambi za muda za wakimbizi wa ndani huko Jamhuri ya Afrika ya Kati. (Picha:UN/Evan Schneider))

Kamati ya UN juu ya haki za watoto kuzitathmini nchi wanachama

Kamati ya Umoja wa Mataifa juu ya haki za watoto, CRC, itatembelea nchi Nne kwa ajili ya kufanya tathmini kama nchi hizo zinatekeleza kikamilifu sheria na kanuni zinazozingatia haki na maslahi ya watoto.

Taarifa ya Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataiaf imesema kamati hiyo iliyokutana kwa wiki kadhaa huko Geneva imesema kuwa nchi zitakazotembelewa ni pamoja na Venezuela,Morocco, Fiji, na Croatia .

Ziara hiyo imepangwa kuanza mwanzoni mwa mwezi ujao.

Ikiwa kwenye ziara hiyo kamati hiyo pia itakuwa na majadiliano na viongozi wa serikali pamoja na wawakilishi wa makundi ya kijamii.

Majadiliano hayo yanatazamiwa kutangazwa moja kwa moja katika mitandao ya kijamii.