Israel yafuta madai ya awali yaliyohusisha UNRWA na mauaji

25 Agosti 2014

Israel imefutilia mbali madai yake ya awali kuwa kombora lililomuua raia mmoja wa Kiisrael lilifyatuliwa kutoka shule moja iliyoko Ukanda wa Gaza ambayo inamilikiwa na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi wa Palestina UNWRWA. George Njogopa na taarifa kamili.

(Taarifa ya George)

Pamoja na kuelezea hali hiyo, UNRWA katika taarifa yake imevitaka vyombo vya habari vya Israel kufanya kazi kwa kuzingatia weledi na siyo kukurupukia mambo.  UNRWA imesema chombo cha habari kilichoarifu juu ya tukio hilo hakikufanya juhudi zozote kujiridhisha na ukweli wa taarifa hizo toka kwa mamlaka husika badala yake kilichukua taarifa za mkondo mmoja.

Taarifa ya UNRWA imevisisitizia vyombo vya habari kubeba jukumu la kupasha habari zenye kuzingatia ukweli na uhalisia wake na kuongeza kuwa chombo hicho pia kinapaswa kuripoti ufafanuzi uliotolewa na jeshi la Israel ambalo limetupilia mbali taarifa hizo za awali.

Ama UNRWA imesema kuwa daima itaendelea kulaani mauaji yanayowalenga watoto kwenye maeneo ya vita ikiwemo pia mauaji ya kijana huyo mwenye umri wa miaka Minne ambaye aliuawa katika eneo la Kusini mwa Israel. Imesema pia inasikitishwa na taarifa za mauaji ya mamia ya watoto huko Palestina.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud