Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wafanyakazi wa kibindamu ni mashujaa:Ban

Wafanyakazi wa usaidizi wa kibinadamu.Picha@UN(videocapture)

Wafanyakazi wa kibindamu ni mashujaa:Ban

Mwaka 2003, tarehe 19 Agosti, wafanyakazi 22 wa Umoja wa Mataifa waliuawa kwenye shambulio lililotokea kwenye  makao makuu ya Umoja huo mjini Baghdad, nchini Iraq. Wengi wao walikuwa ni wasaidizi wa kibindamu waliokuwa wanajitolea kusaidia wenzao.

Tangu siku hiyo, Umoja wa Mataifa unaadhimisha siku ya wasaidizi wa kibinadamu kwa kukumbuka waliouawa na pia kutambua ushuhuda wao katika hatari za kazi hizo.

Mwaka huu, wakati wa maadhimisho yaliyofanyika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, New York, Katibu Mkuu wa Umoja huo Ban Ki-moon amesisitiza kwamba wafanyakazi hao wanaweka maisha yao hatarini kwa ajili ya kusaidia na kuokoa maisha ya wenzao, wakiwa ni mashujaa wa usaidizi wa kibinadamu.

Basi, kwa mengi zaidi kuhusu maadhimisho ya siku ya wasaidizi wa kibinadamu, na kuhusu ushuhuda wa mashujaa hawa Afrika ya Mashariki, ungana na Priscilla Lecomte katika Makala hii.