Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM na Liberia kushirikiana kuhakikisha waathirika wa Ebola wanapata usaidizi

Mfanyakazi kutoka wizara ya afya nchin Liberia akipulizia dawa kiatu cha mwenzake kama njia ya kujikinga na Ebola baada ya kuhudumia kliniki ya wagonjwa wa Ebola mjini Monrovia. (Picha:UNMIL Photo/Staton Winter)

UM na Liberia kushirikiana kuhakikisha waathirika wa Ebola wanapata usaidizi

Ujumbe andamizi wa Umoja wa Mataifa umehitimisha ziara yake hukoLiberiakuangalia hali halisi ya ugonjwa wa Ebola na kusema kuwa taasisi hiyo itahakikisha waathirika wa jangahilowanapata mahitaji muhimu.

Kauli hiyo ni ya Dokta, David Nabarro Mratibu mwandamizi wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ebola aliyotoa wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Monrovia siku ya Alhamisi ambapo aliulizwa kile ambacho Umoja wa Mataifa kinaweza kufanya kuhakikishia usalama wa wale waliowekwa kwenye karantini kuzuia ugonjwa huo na ambao sasa  baadhi wanakabiliwa na ghasia.

(Sauti ya Dkt. Nabarro)

Tutafanya kazi na Serikali kuhakikisha kuwa watu ambao kwa njia moja au nyingine maishayaoyameathiriwa na Ebola watapata chakula, huduma ya Afya na mahitaji mengine ya kimsingi. Lengo la kuongeza juhudi za operesheni  zetukamanilivoelezea  kuwa zinahusisha mashirika mengi ya Umoja wa Mataifa ni kuhakikisha kuwa madhara yanayotokana na mambukizi ya Ebola yanashughulikwa kwa ufasaha. 

WHO imesema kwa ujumla hali ya Ebola bado ni ngumu kutokana na vile ugonjwa huo  umeenea nchi zaidi ya moja na haikutarajiwa lakini ni ugonjwa ambao unaweza kudhibitiwa kwa kutoa huduma sahihi kwa mgonjwa na wengine kujikinga..

Wakati wa ziarayaowamekuwa na mazungumzo na viongozi waandamizi waLiberiaakiwemo Rais Ellen Johnson- Sirleaf, wataalamu wa afya na mashirika yasiyo ya kiserikali.

Ziara ililenga kujifunza kinachoendelea ikiwemo changamoto na kuona kile ambacho kinapaswa kufanywa na Umoja wa Mataifa kwa mshikamano na Liberia kumaliza tatizo la Ebola. Kutoka Liberia, watakwenda Guinea, Sierra Leone na Nigeria