Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwaka mmoja baada ya shambulio huko Ghouta, mzozo wa Syria lazima umalizwe:Ban

UN Photo/Mark Garten)
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.

Mwaka mmoja baada ya shambulio huko Ghouta, mzozo wa Syria lazima umalizwe:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesema jamii ya kimataifa ina wajibu wa kuungana na kumaliza mzozo wa Syria wakati huu kwani madhara yake kwa jamii inaongezeka kila uchao na hata kuvuka mipaka na kuingia nchi jirani.

Katika taarifa yake ya kumbukizi ya mwaka mmoja tangu kufanyika kwa shambulio lililotumia silaha za kemikali huko Ghouta nchini Syria, Ban amesema hata baada ya kitendo hicho mzozo wa Syria bado unaendelea akisema kitendo cha Ghouta kilikuwa ni cha kutisha.

Kwa mara nyingine tena ametuma salamu za rambirambi kwa familia zilizopoteza wapendwa wao kwenye tukio hilo akitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kukumbuka wale waliopoteza maisha katika tukio hilo la kikatili.

Ban amesema mzozo wa Syria umechochea pia ukiukwaji wa haki za binadamu na uhalifu dhidi ya binadamu na kusababisha hata kuenea kwa ugaidi.

Katibu Mkuu amesema yeye kupitia Umoja wa Mataifa na mjumbe wake maalum kuhusu Syria watafanya kila wawezalo kumaliza vita inayoendelea Syria