Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Benomar afanya mazungumzo na viongozi wa kisiasa nchini Yemen

UN Photo/Eskender Debebe
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Yemen Jamal Benomar. Picha:

Benomar afanya mazungumzo na viongozi wa kisiasa nchini Yemen

Mshauri maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Yemen Jamal Benomar amekuwa na mashauriano na Rais Abed Rabbo Mansour Hadi wa nchi hiyo ili kufikia suluhu ya kudumu kupitia kwa mazungumzo. Taarifa zaidi na Amina Hassan.

(Taarifa ya Amina)

Mshauri huyo amesema anafanya mazungumzo ya kina na viongozi wengi wa kisiasa na vyama nchini ili kufikia makubaliano ya jinsi ya kupata suluhu kwa mgororo kwa mantiki ya Mazungumzo ya Kitaifa, akiongeza kuwa atafanya kila jitihada kuhakikisha chanzo cha machafuko Yemen kinakabiliwa.

Benomar amesihi wahusika wote kuonyesha hekima na ushirikiano wa kitaifa ili kukabiliana na changamoto ya sasa kwa minajili ya kusukuma mbele mchakato mzima wa kisiasa.

Mathalani amesisitiza umuhimu wa kutii makubaliano ya mpito, matokeo ya mashauriano ya kitaifa pamoja na maazimio ya Baraza la Usalama.

Benomar amemhakikishia Rais Hadi usaidizi wa Umoja wa Mataifa na jamii ya kimataifa katika juhudi kupatia msukumo kipindi cha mpito cha kisiasa, ulinzi wa amani, na utulivu nchini Yemen