Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi za visiwa vidogo zinazoendelea zahitaji ubia endelevu

Nchi za visiwa vidogo zinazoendelea zahitaji ubia endelevu

Ikiwa zimebakia takribani wiki  mbili kabla ya kuanza kwa mkutano wa tatu wa Umoja wa Mataifa kuhusu nchi za visiwa vidogo, SIDS, huko Apia, Samoa, Katibu Mkuu wa mkutano huo Wu Hongbo amesema ubia endelevu ni moja ya mambo muhimu ya kuwezesha maendeleo ya kudumu kwa maeneo hayo.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini New York, Wu amesema ubia wa aina hiyo ni ili kuleta mabadiliko dhahiri kwenye nchi hizo zinazokumbwa na matatizo kutokana na jiografia zao na hata upatikanaji wa rasilimali.

Bwana Wu ambaye pia ni Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya uchumi na kijamii akataja mambo mengine muhimu yatakayopatiwa kipaumbele kwenye mkutano huo.

(Sauti ya Wu)

"Jamii ya kimatiafa kwa pamoja iko tayari kushughulikia mambo au changamoto zinazozikabili SIDs. Changamoto za SIDs ni changamoto za ulimwengu mzima. Ujumbe wa pili ni kwamba tunawajali kama jamii ya kimataifa, na kama Umoja wa Mataifa. Kwa hivyo si jambo la kawaida kwa nchi wanachama kufikia makubaliano kwenye nyaraka inayokuwa na viashiria vya kisiasa hata kabla ya kongamano. Hii ni ishara ya yale tunayoweza kufanya kwa pamoja."

Halikadhalika amesema mwisho mwa mkutano huo kutatolewa nyaraka maalum ambapo nchi za SIDS zimependekeza kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa awe anatoa ripoti ya ufuatiliaji na utekelezaji.

SIDS ina nchi wanachama 39 zikiwemo Comoro,Cape Verde,Seychelles,Guinea-BissaunaMauritius.