Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msaada wa Kuwait kwa WHO waokoa wahanga wa vita Syria

Picha@UN WHO

Msaada wa Kuwait kwa WHO waokoa wahanga wa vita Syria

Shirika la afya duniani, WHO limesema msaada ya dola Milioni 45 kutoka serikali ya Kuwait umeokoa maisha kwa kushughulikia mahitaji ya kiafya ya mamilioni ya watu walioathiriwa na vita nchini Syria.

Ripoti mpya ya WHO kuhusu matumizi ya fedha hizo imesema msaada umetumika katika huduma muhimu za afya katika eneo linaloshikiliwa na serikali ya Syria na wapinzani pamoja na kusaidia wakimbizi Milioni 2.9 wa Syria waliopo Misri, Iraq, Jordan, Lebanon na Uturuki.

WHO iliwasilisha ripoti hiyo kwa serikali ya Kuwait ambapo inaeleza kuwa ilisambaza dawa muhimu kwa mamilioni ya watu waliogua magonjwa sugu kama figo, kifafa, pumu, na ugonjwa wa kisukari, halikadhalika vifaav ya upasuaji kwa ajili ya majeruhi.

Kwa Syria pekee, usaidizi wa Kuwait uliwezesha watu zaidi ya Milioni Mbili wanaoishi kwenye majimbo 13 yanayoshikiliwa na serikali na wapinzani kupata dawa za kukoa maisha pamoja na matibabu ya akili.