Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Huduma za afya Iraq, WHO yapata usaidizi kutoka Saudi Arabia

Huduma za afya Iraq, WHO yapata usaidizi kutoka Saudi Arabia

Shirika la afya duniani, WHO limepata msaada wa dola Milioni 49 kutoka Saudi Arabia kwa ajili ya kuimarisha huduma ya afya kwa mamilioni ya watu walioathiriwa na mzozo unaoendelea nchini Iraq.

Msaada huo wa Saudi Arabia, ambao ni kiasi kikubwa cha msaada kuwahi kutolewa na taifa moja kwa WHO kwa minajili ya mgogoro maalum, utasaidia juhudi za shirika hilo katika kupambana na mlipuko wa magonjwa, utapiamlo, upungufu wa dawa na pia kupunguzia mzigo kliniki na hospitali.

Paul Garwood ni msemaji wa WHO Geneva.

(Sauti ya Paul)

Tunashukuru sana kwa msaada wa saudi arabia, sasa utowaji wa chango dhidi ya polio utaongezeka kwa zaidi ya asilimia 94, na huu ni mmoja tuu ya mifano ya jinsi msaada huu utakavyosaidia”

Ongezeko la mapigano ya hivi karibuni huko Iraq, uhamiaji mkubwa wa watu na kuwepo kwa wakimbizi 250,000 kutoka nchini Syria kumesababisha mifumo ya huduma za afya nchini Iraq kuelemewa.