Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban alaani mauaji ya mwandishi wa habari Foley

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.Picha/UM

Ban alaani mauaji ya mwandishi wa habari Foley

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali mauaji ya kikatili ya mwandishi wa habari James Foley.

Taarifa ya msemaji wa Umoja wa Mataifa imemkariri Ban akisema kuwa kitendo hicho kibaya ni ishara ya kampeni ya ugaidi inayoendeshwa na kikundi cha waislamu wenye msimamo mkali ISIL dhidi ya wananchi wa Iraq na Syria.

Ametuma salamu za rambirambi kwa familia, marafiki na wafanyakazi wenzake marehemu Foley huku akitaka watekelezaji wa kitendo hicho na uhalifu mwingine wafikishwe mbele ya sheria.