Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatujasahau wasichana wa Chibok, Nigeria: UNFPA

UN Photo/Loey Felipe
Mkuu wa UNFPA nchini Nigeria Bi. Ratidza Ndhlovu,

Hatujasahau wasichana wa Chibok, Nigeria: UNFPA

Shirika la idadi ya watu duniani, UNFPA limesema halijasahau mahitaji ya wanawake na wasichana huko Chibok, Kaskazini mwa Nigeria ambako kundi la Boko Haram limekuwa tishio na kuharibu harakati za maisha ya kila siku ya jamii.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini New York, Mkuu wa UNFPA nchini Nigeria Ms. Ratidza Ndhlovu amesema usaidizi huo ni pamoja na huduma za afya ya uzazi na ushauri nasaha kwa watoto wa kike waliokumbwa na vitendo vya ubakaji wakati wakitoroka kutoka kwa wanamgambo hao wa Boko Haram.

Amesema utoaji wa misaada hiyo unakumwbwa na changamoto kwa sababu hofu iliyotanda imesababisha maelfu kukimbia makwao hususan kwenye mji mkuu wa jimbo la Bono, Maiduguri.

(Sauti ya Bi. Ndhlovu)

Changamoto tunayokumbana nayo kwa watu watu waliokimbia makwao ni kwamba baadhi yao hawapendi kwenda kuishi kwenye kambi kwa kuwa ni hatari kwa maisha yao. Hii ni kwasababu waasi wanapenda mikusanyiko ya watu na hivyo watu hawapendi kukaa kwenye makundi na hivyo wanakwenda kusaka hifadhi kwa wenyeji, jambo linaloweka shinikizo kwa baadhi ya familia hizo.”

Mkuu huyo wa UNFPA Nigeria ametaja changamoto nyingine kuwa washauri nasaha waliopatiwa mafunzo nao wanaondoka na hivyo kusababisha utoaji wa mafunzo uwe ni endelevu.