Siku ya usaidizi wa kibinadamu: Tuangazie pia udhibiti wa migogoro: Ashe

19 Agosti 2014

Katika kuadhimisha siku ya wasaidizi wa kibinadamu ulimwenguni leo Agosti 19, Umoja wa Mataifa umewakumbuka wafanyakazi wote waliopoteza maishayaowakitafuta amani duniani wakiwemo 22 waliofariki dunia katika shambulizi la bomu kwenye makuu ya Umoja huo mjiniBaghdad,Iraqmwaka jana.

Rais wa Baraza Kuu la Umoja huo John Ashe katika ujumbe wake wa siku hii amesema kila siku maelfu ya wafanyakazi wa msaada ya kibinadamu wanazidi kuhatarisha maishayaowakati wakisaidia watu walio na mahitaji muhimu.

Hivyo amesema siku hii sio fursa tu kuadhimisha kujitolea kwa wafanyakazi hao, bali pia ni nafasi ya kuangazia umuhimu wa kuchukua hatua zaidi kwani ongezeko la migogoro limeendelea kutishia jamii za mamilioni ya watu ambako maisha yamesambaratika kutokana na vita na mjangaa ya kiasili.

Ashe amesema wakati dunia inapanga kutekeleza  agenda endelevu ya kuangamiza umasikini sambamba na kuwa na jamii yenye amani, mtazamo jumuishi wa jamii ni muhimu ili kuwepo na mafanikio na kujenga jamii inayozingatia haki ya wote kwa manufaa ya kila binadamu.