Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tanzania imeshuhudia upungufu, maambukizi ya ukimwi kutoka kwa mama hadi mtoto

UN Photo/B Wolff
Mama amnyonyesha mwanawe nchini Tanzania.

Tanzania imeshuhudia upungufu, maambukizi ya ukimwi kutoka kwa mama hadi mtoto

Upatikanaji wa huduma ya afya kwa watoto umekumbwa na changamoto kwa miaka mingi, hivyo kusababisha maafa kwa watoto kabla kutimiza umri wa miaka mitano. Wakati nchi kwa ushirikiano na mashirika mbalimbali zikijikita katika kukabiliana kuepusha vifo vya watoto wachanga, maafa kutokana na maambukizi ya ukimwi kutoka kwa mama hadi mtoto yameripotiwa kupungua katika nchi nyingi.Tanzania ni moja ya nchi ambazo zimeshuhudia mafanikio hayo . Basi ungana na Mansouri Jumanne wa Radio washirika Radio SAUT ilioko, Mwanza, Tanzania.