Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yaanza kusambaza Misaada ya Kibinadamu nchini Libya

Misaada ya kibinadamu imewasili Libya.Picha@© UNHCR/A.Ibrahim

UNHCR yaanza kusambaza Misaada ya Kibinadamu nchini Libya

Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR, kwa ushirikiano na wadau wake ikiwemo wahudumu wa Afya wa Kimataifa (IMC) na shirika la Taher Al Zawia wametuma misaada kwenda kwa maelfu ya watu waliofurushwa kutoka makazi yao baada ya mapigano yanayoendelea karibu na mji mkuu Tripoli nchini Libya.

Zaidi ya jamii 2,000 zinahitaji misaada ya dharura hususan matibabu na dawa, blanketi , vyakula na magodoro.

Misaada hiyo itafikia watu hao waliosaka hifadhi katika mji wa Zawiya ulioko kilometa 45, magharibi mwa Tripoli.

Kaimu mkuu wa UNHCR nchini Libya Saado Qoul amesema kuwa operesheni hiyo imetekelezwa kwa wakati ambao duru zinaeleza kuwa hali ya wakimbzi hao iko mbaya zaidi.

Amedema anatarajiwa misaada zaidi itapelekwa ili kuokoa maisha ya watu hao.

Bwana Quol emsema UNHCR ina ghala la misaada muhimu mjini Tripoli lakini kwa sababu ya mapigano yanayoendelea, imekuwa vigumu kulifikia.