Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Benki ya Dunia kuboresha maisha ya wakimbizi na jamii zinazowahifadhi Afrika

Washauri wa Benki ya Dunia katika kambi ya Kiryandongo. Picha ya John Kibego.

Benki ya Dunia kuboresha maisha ya wakimbizi na jamii zinazowahifadhi Afrika

Benki yaDunia imeanza safari ya kutafuta suluhu ya kudumu kwa matatizo yanayowakumba wakimbizi na jamii zinazowahifadhi barani Afrika. Kwa sasa inapanga kuanzisha miradi kabambe ya kusaidia wenyeji na wakimbizi kujiimarisha kiuchumi. John Kibego wa radio wahsirika ya Spice FM, ameongea na Washauri wa benki hiyo waliotembelea kambi ya Kiryandongo nchini Uganda.

(Taarifa ya Kibego)

Baada ya kutathmini uwezekano wa uwekezaji huo katika maeneo ya Sahel na lile la Maziwa Makuu, sasa wanatembelea nchi za Pembe mwa Afrika zikiwemo Somalia Ethiopia na Eritrea.

Miradi inayolengwa ni pamoja na ujenzi wa viwanda vidogo vidogo, miundombinu kama hospitali na vyuo vya kiufundi, ili watu wabadilike kiuchumi, waweze kujitegemea badala ya misaada ya kibinadamu.

Finn Skadkaer Pedersen ni Mshauri Mwandamizi wa Benki ya Dunia kuhusu mpango huu.

(Sauti ya Finn Skadkaer Pedersen)

Alice Litunya Mkuu wa Ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) ya Hoima, ameonyesha matumaini yake kuhusu mkakati huo.

(Sauti ya Alice Litunya)

Bwana Pedersen amesema, mpango huo pia unaangazia wakimbiizi wa ndani, jamii zinazowahifadhi na maisha baada ya ukimbizi.