Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tatizo la afya ya akili lilikuwa ni mada kuu, Siku ya vijana duniani

Vijana wakiwa makao makuu ya UM,waakti wa kongamano la vijana.Picha ya UM/Mark Garten.(maktaba)

Tatizo la afya ya akili lilikuwa ni mada kuu, Siku ya vijana duniani

Matatizo ya akili kwa vijana husababisha unyanyapaa na ubaguzi, ambavyo aghalabu vinatokana na kutokuwepo uelewa mwema wa matatizo ya afya ya akili. Kwa mujibu wa Katibu Mkuu Ban Ki-moon, unyanyapaa unaohusiana na matatizo ya afya ya akili unaweza kuchangia kuwatenga waathiriwa au kuwafanya wakate tamaa katika kutafuta usaidizi, wakiogopa kuhusishwa na sifa mbaya.

Katika kuadhimisha Siku ya Vijana Duniani mwaka huu, lilifanyika kongamano la vijana hapa kwenye Umoja wa Mataifa,kamasehemu ya juhudi za kukabiliana na unyanyapaa huo ili kuhakikisha kuwa vijana wenye matatizo ya afya ya akili wanaishi maisha ya afya, yaliyokamilika na bila kutengwa na kudhalilishwa, na waweze kutafuta huduma na usaidizi wanaohitaji.