Ban asema uamuzi wa Al Malik ni wa kuungwa mkono

15 Agosti 2014

Katibu mkuu wa Umoja w a Mataifa Ban Ki-moon amepongeza uamuzi wa Waziri Mkuu wa Iraq Bwana Nouri Al Maliki wa kukubali kujitoa katika kinyang’anyiro cha kiti cha Uwaziri Mkuu na badala yake kumuunga mkono Waziri mkuu mteule Bwana Heiner Al Abbadi kama mrithi wake. John Ronoh na ripoti kamili.

(Taarifa ya John)

Ban amesema katika taarifa kupitia msemaji wake kuwa hii itaruhusu mpango wa kuunda serikali mpya kuendelea kwa kasi kulinganana na wakati uliowekwa kikatiba.

Amemshukuru Bwana al- Maliki kwa uamuzi huo na akaitaja kuwa njia bora ya kukabidhi uongozi kwa kanuni za kikatiba na amewasihi viongozi wa kisiasa nchini Iraq kutumia wakati huu wa kihistoria kushirkiana na kujenga maafikiano yao ili kuharakisha mbinu za kutafuta suluhu wa changamoto nyingi zinazokabili nchi hiyo.

Ameendelea kusema kuwa anatarajia kuundwa haraka kwa serikali jumuishi itakayounganisha raia wote wa Iraq ili kuwezesha kutatua shida zote mara moja.

Naye Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu na Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq Nickolay Mladenov, leo ameukaribisha uamuzi huo wa al-Maliki wa kuunga mkono Rais Fuad Mansoum kwa kumchagua Dokta Haider al-Abbadi kwa jitihada za kuunda serkali mpya nchini humo.

Amesema uamuzi huo unadhihirisha uongozi bora na kujitolea kutegemeza mpango wa kidemokrasia na heshima ya katiba.

Bwana Mladenov amemshukuru waziri mkuu huyo anayeondoka kwa msimamo wake wa kushirikiana na Umoja wa mataifa kwa miaka mingi na hivyo kumtakia mema, akimhakikishia kuwa Umoja huo utaendelea kufanya kazi naye katika siku za usoni.