Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Miji inayojaribu kuhimili majanga ya hali ya hewa yafika 2000

UN Photos/Evan Schneider
mafuriko nchini Pakistan @

Miji inayojaribu kuhimili majanga ya hali ya hewa yafika 2000

Idadi ya miji iliyojiunga na mtandao wa kampeni ya Umoja wa Mataifa ya kukabiliana na hatari za tabianchi imefikia 2000.

Kampeni iliyozinduliwa mwaka 2010 iitwayo Making Cities Resilient: My City is Getting Ready! inalenga kuelimisha viongozi kuhusu hatari zitokanazo na hali ya hewa kama vile mafuriko au maporomoko ya ardhi, na kubadilisha mifumo ya ujenzi wa miji.

Masharti 10 ya mtandao huo ni pamoja ya kujenga miundombinu ya kupunguza hatari hizo, kurekebisha majengo ya shule na hospitali ili zilindwe na mafuriko na hatari zingine, kuunda mifumo ya tahadhari na kadhalika.

Asilimia 25 ya miji iliyojiunga na mtandao huo ipo Amerika ya Kusini lakini tayari miji tisa ya Afrika ya Mashariki imejiunga na kampeni hii, ikiwemo Moshi Tanzania, Nairobi, Narok na Kisumu Kenya, Bujumbura Burundi, Wilaya ya Bukedea, Entebbe na Kampala nchini Uganda.