Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vifo vya watoto wachanga bado changamoto Tanzania

Baby Nyariek@Picha Unifeed

Vifo vya watoto wachanga bado changamoto Tanzania

Lengo la nne ya Malengo ya Maendeleo ya Milenia ni kuhakikisha kwamba huduma za afya zinapatikana kwa raia ili kutokomeza vifo vya watoto wachanga. Huko Mwanza Tanzania, changamoto nyingi zinawakumba wanawake wajawazito kwa sababu ya kutokuwepo kwa zahanati na hospitali karibu na makazi yao husususan vijijini. Je wanawake wajawazito wana maoni yapi kwa ajili ya shida zinazowakumba? Wahudumu nao wanatarajia jambo hili litatatuliwa na serikali kwa njia gani? Basi ungana katika makala hii na Mansouri Jummane kutoka radio washirika Radio SAUT, Mwanza Tanzania.