Wataalamu wa UM kuzuru Azerbaijan

14 Agosti 2014

Jopo la wataalamu huru wa Umoja wa Mataifa linatazamiwa kuzuru nchini Azerbaijan kuanzia Agosti 18 mwaka huu kwa ajili ya kuendesha uchunguzi kuhusiana na uvunjifu wa haki za binadamu.

Jopo hilo ambalo hii itakuwa ni ziara yake ya kwanza kufanya  nchini humo litakuwa na jukumu la kuangalia namna shughuli za kibiashara zinavyokiuka haki za binadamu.

Akizungumza kabla ya kuanza ziara hiyo itayodumu hadi Agosti 27, mmoja wa wajumbe kwenye jopo hilo Puvan Selvanathan,amesema kuwa wakati huu ambapo taifa hilo linachipua kwa kasi katika sekta za mafuta, kumejitokeza changamoto nyingi ambazo zinabinya haki za binadamu kutokana na kupanuka kwa shughuli za kibiashara.

Wataalamu hao pamoja na mambo mengine watatathmini nanma taifa hilo linavyotekeleza msingi ya Umoja wa Mataifa inayohusu biashara na haki za binadamu.

Wakiwa nchini humo wataalamu hao watakuwa na mazungumzo na maafisa wa serikali na baadaye kutembelea mji wa pili kwa ukubwa wa Ganja kabla ya kukutana na waandishi wa habari.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter