Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mfumo dume watukwaza; wasema wanawake Tanzania

Picha@ Rashidi Chilumba, Radio SAUT

Mfumo dume watukwaza; wasema wanawake Tanzania

Usawa wa kijinsia ni tatizo huko Mwanza nchini Tanazania ambapo wajane wanakumbwa na tatizo hilo kwa kunyang'anywa mali walizochuma na waliokuwa waume zao. Je matatizo yapi huwapata? na je hali ya kujenga uwezo kwa  wanawake  na kutokomeza mfumo huo dume ili kuwezesha utimilifu wa lengo la tatu maendeleo ya milenia la  Usawa wa Kijinsia inatekelezwa vipi nchini Tanzania? Basi ungana katika makala hii na Rashidi Chilumba kutoka Radio Washirika Radio SAUT ya MwanzaTanzania.