Kurekebisha uchumi na mabadiliko ya tabianchi kutaleta maendeleo: UNEP

13 Agosti 2014

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Mazingira UNEP limetoa ripoti mpya inayoonyesha kwamba uwekezaji pesa katika kubadilisha uchumi wa nchi za kiafrika unaweza kuzuia kasoro za mabadiliko ya tabianchi bali pia kuleta maendeleo endelevu .

Achim Steiner, mkuu wa UNEP, amekumbusha kwamba asilimia 94 ya kilimo cha Afrika kinategemea maji ya mvua, na mavuno yanaweza kupungua kwa asilimia 15 hadi 20 ifikapo 2050 kutokana na mabadiliko ya tabianchi.

Kwa hiyo ni lazima kupata njia mbadala ya kurekebisha uchumi wa nchi hizo, na ripoti hiyo inalenga kutoa mifano yenye gharama ndogo ili kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa. Nchini Rwanda na Uganda, kwa mfano, serikali zimetekeleza miradi ya kilimo bora kwa kupanda miti na kutumia mpango wa umwagiliaji maji, kwa kuwekeza dola 13 tu kwa kila mtu.

Richard Monang, ni mtalaam wa UNEP aliyeandika ripoti hiyo…

(Sauti ya Monang)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud