Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kenya yachukua hatua kudhibiti uwezekano wa mlipuko wa Ebola

Harakati za kujikinga dhidi ya Ebola. (Picha@WHO)

Kenya yachukua hatua kudhibiti uwezekano wa mlipuko wa Ebola

Shrika la afya duniani, WHO limesema Kenya iko hatarini kukumbwa na maambukizi ya ugonjwa wa Ebola kwa kuzingatia kuwa ni kitovu cha usafiri wa ndege kutoka Afrika Magharibi. John Ronoh na ripoti kamili.

(Taarifa ya John)

Hili ni onyo la kwanza kutolewa na WHO siku chache baada ya kuridhia matumizi ya dawa ya majaribio kutibu ugonjwa huo.

Kufuatia onyo hilo Idhaa hii imezungumza na Mkurugenzi wa huduma za afya katika Wizara ya afya nchini Kenya Dokta. Nicholas Muraguri ambaye amesema tayari wamechukua hatua kuelimisha umma ili kuondoa wasiwasi

(Sauti ya Dkt Muraguri)

Tangu ulipuke Afrika Magharibi mwezi Machi kwenye nchi za Guinea, Liberia, Sierra Leone na Nigeria kwa sasa Ebola imeua zaidi ya watu Elfu Moja, ukielezwa kuwa ndio mlipuko mkubwa zaidi na wenye kutatanisha zaidi.