Siku ya Tembo Duniani yatukumbusha hatari zinazowakumba:UNEP

12 Agosti 2014

Takribani tembo 25,000 huuawa kila mwaka miongoni mwa idadi nzima ya tembo kati ya 420,000 na 650,000 waliopo duniani.

Ni kwa mujibu wa Shirika la Mpango wa mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP, likiadhimisha siku ya tembo duniani Agosti 12 ikiwa ni mwaka wa tatu huku likikumbusha dunia kuwa iwapo ujangili utaendelea tembo watatoweka duniani.

UNEP imetaja sSababu ya kwanza ni mahitaji ya pembe za ndovu yanazidi kuongezeka duniani kote, hasaAsia, yakikadiriwa kuwa biashara yenye thamani ya dola milioni 165 hadi 188 kila mwaka.

Imesisitiza kwamba hatari hiyo inaweza kukabiliwa, hatua mbali mbali zikichukuliwa mfano, kuacha kununua bidhaa zilizotengenezwa na pembe hizo ama kufadhili mashirika yanayojihusisha na kupambana na ujangili wa tembo.

Aidha UNEP imesema itaendelea kuelimisha jamii kuhusu athari za ujangili kwa maisha ya tembo na mazingira ya ulimwengu kwa ujumla.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud