Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNSMIL yatoa wito kwa pande kinzani Libya ziunge mkono juhudi za kusitisha mapigano

Nembo ya UNSMIL

UNSMIL yatoa wito kwa pande kinzani Libya ziunge mkono juhudi za kusitisha mapigano

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya, UNSMIL, umelaani vikali mapigano yanayoendelea mjini Tripoli, licha ya wito uliotolewa mara kwa mara wa kusitisha mapigano mara moja na kutotumia nguvu kutatua tofauti za kisiasa. Ujumbe huo umetoa wito kwa pande zinazozozana kuunga mkono juhudi za kusitisha mapigano mara moja.

UNSMIL imelaani pia kuongezeka idadi ya raia wanaouawa na kuelezea kusikitishwa na uhaba wa vifaa vya matibabu, maelfu ya familia kulazimika kuhama makwao, uharibifu mkubwa wa nyumba za watu na miundo mbinu, pamoja na kusitishwa shughuli za kiuchumi.

Ujumbe huo pia umelaani mapigano yanayoendelea eneo la mashariki mwa nchi, ambayo yanawadhuru raia, na mashambulizi dhidi ya vituo vya polisi na jeshi, pamoja na kutumia ndege za kijeshi katika mapigano.