Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya kibindamu mlima Sinjar ni mbaya; baadhi wajinasua:OCHA

Wakimbizi wa ndani wavuka kutoka Sahela wakielekea hadi maeneo salama ya Zummar.Picha@UNHCR

Hali ya kibindamu mlima Sinjar ni mbaya; baadhi wajinasua:OCHA

Ikiwa ni siku ya Tisa tangu watu wa jamii ya Yazed na makundi madogo wajifiche kwenye mlima Sinjar huko Iraq wakikimbia mashambulizi dhidiyaokutoka kikundi cha waislamu wenye msimamo mkali ISIL , Umoja wa Mataifa umesema haliyaoya kibinadamu inazidi kudorora kila uchao.

Mkuu wa mawasiliano wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu, OCHA Kieran Dwyer amewaambia waandishi wa habari kuwa mamia ya maelfu ya jamii hizo wako kwenye hali mbaya lakini vyakula vinavyodondoshwa kwa ndege vimekuwa na msaada kwani wakati huu mazingira ni magumu.

(Sauti ya Dwyer-1)

Watu walionasa mlimani bila shaka wanakabiliwa na joto kali, tunazungumzia nyuzi joto 45 kwa kipimo cha Selsiyasi. Watu hao wamenasa katika maeneo mbali mbali ya mlima huo na kwa upande wa Kusini ndio wanakabiliwa zaidi na kikundi hicho chenye silaha.”

Hata hivyo amesema baadhi wameweza kujinusuru na hali hiyo..

(Sauti ya Dwyer-2)

Tunaweza kuthibitisha kuwa katika saa 72 zilizopita maelfu ya watu wameweza kukimbia kutoka mlimani kwa usaidizi wa vikosi vya usalama vya Kurdi na wengineo. Wengine wanakimbia kutoka upande wa kaskazini mwa mlima ambao ni karibu na mpaka na Syria. Kutoka hapo wanatembea kwa mguu kwa saa Saba au wakati mwingine kwa gari hadi kwenye mto Tigris na hatimaye wanaingia Iraq.”

OCHA imesema tangu ISIL waimarishe mashambuliziyaotarehe Tisa Juni mwaka huu, zaidi ya watu Laki Sita wamepoteza makaziyaona kufanya idadi ya wakimbizi wa ndani nchiniIraqifikie zaidi ya Milioni moja nukta Mbili.