Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama ziarani Ulaya na Afrika

Baraza la Usalama.Picha ya UM//Paulo Filgueiras/NICA

Baraza la Usalama ziarani Ulaya na Afrika

Wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, wameanza ziara yao ya Ulaya na Afrika kwa kutua kwanza Ubeljiji na The Hague, Uholanzi, kabla ya kuelekea Sudan Kusini na Somalia.

Wakiwa The Hague, walikutana na wawakilishi wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai, ICC, Mahakama ya Sheria ya Kimataifa, ICJ na majopo maalum ya sheria na Shirika la Kupinga Silaha za Kemikali, OPCW.

Kwenye ICC wamejadili kuhusu mchango wa mahakama hiyo na jinsi majukumu yake yanashabihiana na yale ya Baraza la Usalama, huku ziara yao huko Ulaya ikiangazia sheria ya kimataifa na uwajibikaji.

Ziara hiyo ya Baraza la Usalama itahitimishwa mnamo Agosti 14.