Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nina matumaini amani itapatikana Darfur: Mkuu wa UNAMID

Dkt. Mohammed Ibn Chambas akihojiwa na Assumpta Massoi. (Picha:Carlos Mathias)

Nina matumaini amani itapatikana Darfur: Mkuu wa UNAMID

Ni zaidi ya miaka Kumi sasa tangu kuanza kwa mzozo huko Sudan kwenye jimbo la Darfur ambako vikundi vya waasi vinapingana na serikali. Watu wamepoteza maisha, wengine kujeruhiwa na hata kupoteza makazi na mali. Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika mwaka 2007 ulianzisha ujumbe wa pamoja UNAMID ambao hivi karibuni mkuu wake Dkt. Mohammed Ibn Chambas alihutubia baraza la usalama kueleza hali halisi. Assumpta Massoi wa Idhaa hii alizungumza naye katika mahojiano maalum kufahahamu hali iko vipi na mustakhbali wa eneo hilo. Kwanza anaanza kwa kuelezea ujumbe wake kwa Baraza la Usalama.