Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sierra Leone yakwamua wasichana waliopata ujauzito shuleni:UNICEF

Mbalu mmoja wa wasichana anayetoa ushauri kwa wenzake Sierra Leone. Picha@UNICEF/Sierra Leone

Sierra Leone yakwamua wasichana waliopata ujauzito shuleni:UNICEF

Shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP lilipotoa ripoti ya mafanikio ya malengo ya milenia, limeonyesha kwamba bado jitihada zinahitajika ili kufikisha usawa kati ya wasichana na wavulana katika kupata elimu ya msingi na ya sekondari.

Moja ya vikwazo kwa wasichana kuendelea na masomo ni mimba za utotoni.  Hata hivyo nchini Sierra Leone, Shirika la Umoja wa MAtaifa la Kuhudumia Watoto UNICEF, linafadhili vituo vya jamii ambapo wasichana waliopata ujauzito shuleni wanapeana ushauri ili kuendelea na masomo hata baada ya kujifungua mtoto.

Ungana na Priscilla Lecomte kwenye makala hii.