Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mapigano yaanza tena Gaza; wakimbizi warejea kusaka hifadhi UNRWA

Mtoto akiangalia nyumba ya jirani akiwa katika vifusi vya nyumba iliyoharibiwa © UNICEF/NYHQ2014-0984/El Baba

Mapigano yaanza tena Gaza; wakimbizi warejea kusaka hifadhi UNRWA

Baada ya kumalizika kiku tatu za sitisho la mapigano huko Gaza, mapigano yameripotiwa kuanza tena katika Ukanda wa Gaza.....

Taarifa zaidi na John Ronoh.

(Taarifa ya John)

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Palestina, UNRWA, limesema raia wa Palestina ambao walirudi makwao wakati wa sitishohilo, wamekimbilia tena kupata hifadhi katika majengo ya UNRWA.

Wakati huo huo, mashirika ya misaada ya kibinadamu yameanza shughuli za kuondoa vifusi vya majengo yaliyobomolewa, na kuibua mabomu yaliyorushwa bila kulipuka, yakiwa ni hatari kubwa kwa watoto, na vilevile kuokota maiti zingine.

Alipozungumza na waandishi wa habari mjini Geneva, msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEf, Chris Tidey, amesema idadi ya watoto waliofariki imefika 447, kwanza umri wa siku 10 hadi 17.

Ameongeza  kwamba, hali ya afya na usafi wa familia inatia wasiwasisana, kutokana na upungufu wa majisafi, hapo akisema:

“ Familia zinahangaika kupata maji safi, kwa ajili ya kunywa na kuwa na usafi unaotakiwa kwa afya. Maji safi ya kunywa, kuoga na kufua yalikuwa ni adimu sana hata kabla ya mzozo, takwimu zikionyesha kwamba asilimia tano tu za maji yaliyopo chini ya ardhi katika ukanda ya Gaza yalikuwa yanafaa kwa mahitaji ya kibinadamu

Amesema makombora yaliyorushwa na Israel yameharibu takriban viwanda vyote vya kusafisha maji ya Gaza, na vya kuzalisha umeme.

Mafuta yanahitajika kwa ajili ya kuendesha jenerata, amesema, lakini Israelhaijaruhusu bidhaa hizi ziingie ndani ya Gaza.