Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ataka serikali ziboreshe maisha na fursa za watu wa asili

Katika mkutano wa watu wa asili.UN/DPI.Picha ya Evan Schneider/NICA

Ban ataka serikali ziboreshe maisha na fursa za watu wa asili

Ikiwa kesho terehe 9 Agosti ni Siku ya Kimataifa ya Watu wa Asili, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, amezitaka serikali zishirikiane na watu wa asili ili kuboresha maisha na fursa zao katika jamii, wakati kongamano la kimataifa kuhusu watu wa asili likikaribia mnamo mwezi Septemba. Taarifa kamili na Amina Hassan

(Taarifa ya Amina)

Katika ujumbe wake, Ban amesema siku hiyo inaadhimishwa mwaka huu wakati muhimu, ulimwengu unapojitahidi kuyafikia malengo ya maendeleo ya milenia, MDGs, kuweka mtazamo wa maendeleo endelevu, na kujiandaa kuafikia mkataba mpya kuhusu tabianchi- vyote hivyo vikitarajiwa mwakani.

Katibu Mkuu amesema watu wa asili wanatakiwa kujumuishwa katika kuweka malengo haya, na wanaweza kuchochea maendeleo. Hata hivyo, amesema hilo linawezekana tu ikiwa haki zao zinalindwa.

Kenneth Deer kutoka Canada ni mmoja wa watu ambao wamekuwa wakipigania haki za watu asili kutambuliwa, na anaeleza hatua walizopiga.

(Sauti ya Kenneth)