Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mjadala wa kitaifa Sudan ni fursa ya kumaliza mizozo inayoendelea: UNAMID

UN Photo/Paulo Filgueiras
Mohamed Ibn Chambas, Mwakilishi wa Pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika. Picha:

Mjadala wa kitaifa Sudan ni fursa ya kumaliza mizozo inayoendelea: UNAMID

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa leo limepokea taarifa kuhusu hali ya usalama na kibinadamu huko Darfur nchini Sudan ambapo Katibu Mkuu amesema changamoto ya sasa ni vile ambavyo jamii ya kimataifa inaweza kushawishi pande zote kwenye mzozo huwa ili zitambue kuwa nguvu za kijeshi na mwendelezo wa hali ya sasa havikubaliki.

Ripoti ya Katibu mkuu ilisomwa na mwakilishi wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika, Mohammed Ibn Chambas ambaye amesema pande zote alizozungumza nazo zinakubali mjadala wa kitaifa uliopendekezwa na Rais Omar Al Bashir.

Amesema licha ya kwamba kuna vipengele vya kushughulikia lakini mjadala huo unatoa fursa hivyo akawasilisha ombi lake kwa Baraza la Usalama…

(Sauti ya Ibn Chambas)

Mkuu huyo wa UNAMID akasema kile ambacho yeye atafanya..

(Sauti ya Ibn Chambas)