Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tanzania na harakati za kutokomeza mila na desturi potovu

Mwanamke mjane Tanzania. Picha:UNICEF/Tanzania

Tanzania na harakati za kutokomeza mila na desturi potovu

Usawa wa kijinsia na kuwezesha wanawake ni lengo namba tatu la maendeleo ya Milenia ikimulika pia kutokomeza tabia za unyanyasaji wanawake hasa wakati waume zao wanapofariki dunia. Nchini Tanzania, harakati zinaendelea kuondokana na mila na desturi potofu zinazokandamiza wanawake. Je hali iko vipi? Basi ungana na Martin Nyoni wa Redio Washirika Redio SAUT kwa makala hii.