Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bei za vyakula zaendelea kupungua duniani: FAO

Kupungua kwa bei ya nafaka kumesaidia kushuka kwa bei ya vyakula.Picha@FAO

Bei za vyakula zaendelea kupungua duniani: FAO

Shirika la Chakula na Kilimo Duniani FAO, limetangaza kipimo cha bei za vyakula kwa mwezi wa Julai kinachoonyesha kushuka  kwa bei za vyakula kwa mwezi wa nne mfululizo.

Akizungumza na Redio ya Umoja wa Mataifa huko Geneva, Mtalaam wa Kiuchumi  Sherin Mustafa amesema, vyakula ambavyo vimeshuka kwa bei hasa ni nafaka, mafuta na bidhaa za maziwa, kwa sababu ya kupatikana kwa wingi, hapo akieleza:

(Sauti ya Sherin)

Kushuka kwa bei kumekuja wakati wa uzalishaji wa kiwango cha juu cha mazao katika mataifa yenye viwango vya juu vya uzalishaji kwa mfano marekani kwa uzalishaji wa mahindi na maharage ya soya, au muunagano wa Ulaya na Oceania katika kuzalisha bidhaa zitokanazo na maziwa

Kwa upande mwingine, bei ya nyama na sukari zimeendelea kupanda, akieleza kwamba sababu ya kwanza ni mahitaji ya watu yanayoendelea kuongezeka kwa bidhaa hizi, na ya pili ni wasiwasi wa soko la vyakula kuhusu mabadiliko ya tabianchi yanayoweza kusababisha mazao machache katika nchi zinazolima miwa, kama vileBrazilnaIndia.

(Sauti ya Sherin)

Taasisi za utabiri wa hali ya hewa zinakadiria kwamba kuna uwezekano wa kuwepo na El nino katika miezi ijayo lakini wakati huo huo makadirio yanaonyesha kwamba athari za mvua hizo hazitakuwa kubwa.”

Bi Mustafa amesema pia kwamba bei za mchele hazikushuka, tofauti na nafaka zingine, kwa sababu Thailand, ambayo ni nchi ya kwanza duniani kwa kuuza mchele, imesimamisha mauzaji yake kutokana na mzozo wa kisiasa unaoendelea nchini humo.