Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pillay aishutumu Japan kwa kushindwa kuwakirimu waathirika wa vita

Navi Pillay. Picha@UNIFEED

Pillay aishutumu Japan kwa kushindwa kuwakirimu waathirika wa vita

Mkuu wa Kamishna ya Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu Navi Pillay ameelezea masikitiko yake kwa Serikali ya Japan ambayo inadaiwa kushindwa kutoa suluhisho la kudumu kwa watumwa wa kingono waliokumbwa na masahibu hayo wakati wa vita, akionya kuwa haki za waathirika hao zinazojulikana kama ‘faraja kwa wanawake’ zinaendelea kuvunjwa kwa miongo kadhaa tangu kumalizika kwa Vita Kuu ya Pili ya Dunia. Taarifa kamili na George Njogopa.

(Taarifa ya George)

Kamishna Pillay amesema kuwa wakati wa ziara yake nchini Japan aliyoifaya mwaka 2010 alitoa mwito kwa serikali ya Japan kutafutiwa ufumbuzi wa kudumu juu ya waathirika hao wa vita, lakini jambo la kushangaza ni kwamba wakati kipindi chake kwenye ofisi hiyo kikielekea ukingoni jambo hilo bado halijashughulikiwa.

Amesema kuwa kuna hali ya kukatisha tamaa tena ya kusikitisha kuona kwamba serikali imeshindwa kuchukua hatua zozote kuwafidia wanawake hao. Amesema wasiwasi mkubwa unaojitokeza ni kwamba idadi kubwa ya waathirika hao wanaendelea kupoteza maisha bila kupata  stahili yoyote

Pillay amesema wanawake hao badala ya kufikiwa na haki zao badala yake wamekuwa wakikumbana na matukio ya ajabu ikiwamo yale ya dhihaka na kusememangwa vibaya toka kwa watu wenye kuheshimika nchini Japan. Ravina Shamdasani ni msemaji wa Ofisi ya Haki za Binadamu mjini Geneva.

(Sauti ya Ravina)