Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Palestina yasaka ushauri wa kujiunga na ICC

Fatou Bensouda,ICC amekutana leo na Riad Al-Malki,waziri wa mambo ya nje wa Palestina

Palestina yasaka ushauri wa kujiunga na ICC

Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Jinai, ICC, Fatou Bensouda, amekutana leo na Riad Al-Malki, ambaye ni waziri wa mambo ya nje wa Palestina, huko The Hague, Uholanzi.

Katika mkutano huo, Waziri Al-Malki ameeleza wasiwasi wake juu ya mapigano yaGazana amemwomba Bi Bensouda maelezo kuhusu jinsi ya kujiunga na Mahakama hiyo.

Lengo la mkutano huo ulikuwa ni kumfahamisha mpango mzima wa mkataba wa Roma na jinsi ya kuridhia mamlaka ya ICC.

ICC imesema Palestina si mwanachama wa Mkataba wa Roma, na ingawa imepewa hadhi ya uangalizi ndani ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Novemba mwaka 2012, ICC haijapokea barua yoyote ya Palestina ya kuitambua mamlaka ya ICC ama kuiomba ifanye uchunguzi juu ya uhalifu wowote.

Kwa hiyo basi ICC haina mamlaka ya kufuatilia uhalifu unaotekelezwa ndani ya maemeo ya Palestina.