UM wasikitishwa na tetemeko la ardhi China

4 Agosti 2014

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ameeleza kusikitishwa kwake na vifo vya watu na kuharibika kwa majengo na miundombinu katika maeneo ya China kusini, kufuatia tetemeko la ardhi lililotokea jimbo la Yunnan, siku ya jumapili.

Taarifa ya msemaji wake imemkariri Ban akituma rambirambi kwa serikali ya China na familia za wahanga huku akiwapa pole majeruhi na wote walioathirika na tetemeko hilo.

Amesema Umoja wa Mataifa uko tayari kutuma msaada wake ili kukidhi mahitaji ya kibinadamu na kuratibu misaada ya kimataifa.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter