Mtoto anyonye maziwa ya mama pekee miezi sita ya mwanzo: UNICEF

4 Agosti 2014

Wakati wiki ya unyonyeshaji watoto maziwa ya mama duniani ikiwa inaendelea Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF limekumbusha umuhimu wa kunyonyesha watoto ili kuepusha vifo vya utotoni.

Akizungumza na Redio ya Umoja wa Mataifa, Mtalaam wa UNICEF kwa ukanda wa Afrika ya Kati, Noel Marie Zagre, amezingatia mambo muhimu matatu.  Mosi kumpatia mtoto maziwa ya mama mara tu anapozaliwa, Pili mama anyonyeshe mtoto hadi anapofikisha umri wa miaka miwili ili kujenga kinga yake na tatu unyonyeshaji pekee kwa miezi sita ya kwanza:

Nataka kusisisitiza unyonyeshaji pekee yake. Inamaana kwamba mtoto mdogo anapaswa kupatiwa maziwa ya mama pekee yake, na asipewe kitu chochote kingine, hata maji, juisi ama chakula chochote. Ndiyo kitu tunachohitaji kusisisitiza, natunaendela kufanya kazi kuhusu sheria za nchi ili kuimarisha tabia hiyo muhimu kwa watoto”

Amesema, UNICEF inajaribu kuelimisha watu kuhusu madhara ya maziwa ya unga, na kuwezesha wanawake wanaorudi kazini kupata nafasi ya kuendelea kunyonyesha watoto wao.

Takwimu za UNICEF zinaonyesha kwamba asilimia 39 tu ya watoto wanapewa maziwa ya mama pekee kwa kipindi cha miezi sita katika nchi zinazoendelea.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter