Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ashtushwa na kuvunjwa kwa sitisho la mapigano

Msemaji wa Umoja wa Mataifa, Stephane Dujarric.Picha ya UM

Ban ashtushwa na kuvunjwa kwa sitisho la mapigano

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon  amelaani vikali kitendi cha kikundi cha Hamas kuvunja sitisho la mapigano huko Ukanda wa Gaza.

Sitisho la mapigano hilo lilitakiwa kuanza asubuhi ya leo Ijumaa kwa kipindi cha saa 72, lakini mapigano yalirejea baada ya ripoti iliyotolewa na jeshi la Israel kudai kwamba askari wawili wa Israel waliuawa na mwingine ametekwa nyara baada ya mwanzo wa sitisho la mapigano.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa, Stephane Dujarric, amesema, ingawa Umoja wa Mataifa hauna njia huru ya kuthibitisha ripoti hiyo,  Katibu Mkuu anahofia uvunjaji huo utakuwa na matokeo ya hatari kwa raia walioko Gaza, Israel na kwingine. Ikitendeka vitendo kama hivyo, Dujarric ameongeza, Hamas haitaaminika tena na Umoja wa Mataifa.

Katibu Mkuu ameomba askari waIsrael aliyetekwa nyara aachiliwe haraka. Halikadhalika, ameeleza kutiwa wasiwasi na mashambulizi yaIsrael yaliyoanza tena dhidi ya raia walioko Ukanda waGaza, watu 70 wakiripotiwa kuuawa kwa siku ya leo tu. Ameziomba pande zote za mzozo zisitishe upya mapigano jinsi ilivyoamuliwa.