Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa walaani mauaji ya wabunge Somalia.

Mwakili maalum wa Katibu Mkuu, Somalia Nicholas Kay.Picha ya UM/Jean-Marc Ferré

Umoja wa Mataifa walaani mauaji ya wabunge Somalia.

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, UNSOM Nicholas Kay, amelaani kuuawa kwa mbunge wa bunge la serikali ya shirikisho nchini humo Sheikh Aden Madeer..

Taarifa ya UNSOM imemkariri Bwana Kay akielezea kusikitishwa na vitendo vya mashambulizi dhidi ya wabunge akisema kuwa mauaji hayo ni njia ya kuhujumu wale wanaojitahidi kuendeleza ujenzi wa Somalia na akasisitiza kuwa wale wanaotekeleza ukatili huo hawatafaulu.

Mwakalishi huyo amewasifu wabunge wa Somalia kwa ujasiri na jitihada zao wakati huu mgumu, na akawahikikishia kuwa Umoja wa Mataifa utaedelea kusimama na Bunge la Serikali hiyo.

Ametuma rambirambi kwa jamii, marafiki na Serikali ya Somalia kwa kumpoteza mbunge huyo, na wakati huo huo, akasema kuwa waliotekeleza mauaji hayo wakamatwe na wafikishwe mbele ya sheria.